Eeebana daaaah!! hapa ilikua ni first year wadau wangu , si mnajua tena ukiwa nyoya mambo yote unayaona magumu ukizingatia hata sup huzijui so mambo unayaona kama ni magumu fulani hivi na vitu kama ivyo ,ni mambo ya elimu hayo ndio yalivyo ila ukishayazoea mambo yanakua mzux ile mbaya, jamaa kanitumia hii picha ambayo tulipiga mwaka huo wa unjuka chuon hapa Tumaini, dah! kwanza nilipoiona tu nilicheka peke yangu manakeee........... hapa tulikua tunasubilia kuingia pindi la Communication skills ambalo watu wengi lilikua linawaboa kwani lilikua linapigwa mida ya mchana saa 8.30 , kutoka kushoto waliosimama ni dada yetu huyo Eliakunda a.k.a Profesa huyo hapo chini, wa juu kutoka kushoto ni Elisante a.k.a Braza Kifumu, President wa Tumaini university (makumira) wa sasa na Lekule. Walio kaa chini kutoka kushoto ni Dogojohnson mmiliki wa hii blog na David almaharufu Mineso, kwa sasa wote wapo mwaka wa pili...... na mapambano yanaendelea.