UNALIJUA HILI/ DID YOU KNOW THIS?

MAMBO YALIKUA POA SANA!!

Ukweli usio fichika mambo yalikua poa sana pindi ile tuna soma maschool ya advance pale bagamoyo na mambo kama hayo kwani kuli kua na shangwe za ukweli za kujiachia kama ulikua hujui si tulikua karibu kabisa na beach ya bahari ya hindi kama mita 100 hivi kutoka maschool so wana tukichoka kusugua kichwa tunaenda kujichanganya na masela kibao wa beach na vitu kama hivyo mambo ya kuogelea, kupiga piga mapicha na mambo kama hayo so leo mwana nangu mwenyewe wa UDOM kaamua kunitumia picha kunikumbusha tulipotoka kama picha hii inavyoonesha, daaah!! hapa wana tulikua kwenye mjiwe mmoja kama mwamba unapatikana baharini kama umeshawai kutembelea bagamoyo utayaona si unaona pembeni kuna miti aina ya mikoko ndipo picha hii tulipopigia siku hiyo....... mwenye kofia ni Dogojohnson na msela pembeni jina lake limenitoka si unajua tena ni kitambo kimepita tangu mwaka 2006 pindi ile ya form 5& 6 so majina baadhi ya wana yanaanza kunitoka(yeye anapiga mambo ya political science kitu kama icho), ila sio issue waliosimama kutoka kushoto ni Kalokola (socilogy) na mwenzake ni Denis Sugwejo( international relation IR) wote wana wapo University of Dodoma (UDOM) na kozi zao kwenye mabano.
picha na mdau wangu wa UDOM