UNALIJUA HILI/ DID YOU KNOW THIS?

SOMENI NA HII

BABA NA MAMA WA

1. BAsi na tukaamua, kujikita kilimoni,
Kilimo cha manufaa, tena huko mashambani,
Na sera tukaitwaa, kilimo kwanza jamani,
Nyenzo muhimu hakuna, nani atawajibika?


2. BAra pamoja na Pwani, hi sera ilisikika,
Ilitokea bungeni, na tena ilisifika,
Vitendo vya mtegoni, maajabu yatufika,
Nyenzo muhimu hakuna, nani atawajibika?


3. NAsi tunawauliza, mlo anzisha hi sera,
Mlisema kutuchuza, shida kutimiza sera,
Hata pweza anaweza, tabiri shida ya sera,
Nyenzo muhimu hakuna, nani atawajibika?


4. MAna tulijua shida, za kilimo zitakwisha,
Tutakua tumeshinda, Afrika sa kuilisha,
Migongo hatutopinda, matrekita kulimisha,
Nyenzo muhimu hakuna, nani atawajibika?



5. MAmbo mbona yale yale, mashambani twateseka,
Na jembe letu teule, la mkono lasifika,
Mtapiga makelele, na sisi tukibweteka?
Nyenzo muhimu hakuna, nani atawajibika?


6. WAlisema midomoni, wakulima tu tabuni,
Sera kuitoa ndani, Kuileta uwanjani,
Bora na wale kunguni, mbong’o ndo simtamani,
Nyenzo muhimu hakuna, nani atawajibika?

7. Akisema taabuni, wamlaghai kwa kanga,
Mwazidi mlubuni, mwanamama mwamuonga,
Mrudi tena bungeni, muende sheria tunga,
Nyenzo muhimu hakuna, nani atawajibika?
Na. ndugu yenu Dogo Johnson