UNALIJUA HILI/ DID YOU KNOW THIS?

AFENDE SELE NA JOH.MAKINI KUNA BIFU?

AFANDE Sele ametambulisha singo mpya ya 'Kingdom' ambayo inafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya muziki jijini Dar es Salaam, lakini amesema wazi kwamba Joh Makini ni mmoja kati ya watu aliowaimba. Mfalme huyo wa Rhymes anasema kuwa ujumbe uliopo kwenye wimbo huo ameuelekeza wazi kwa msanii huyo kwa madai kuwa anatumia maneno machafu katika nyimbo zake ambayo yanashusha hadhi ya muziki huo. Msanii huyo ambaye ni shabiki wa Simba, alitolea mfano wimbo wa 'Niaje Nivipi' ambao amedai Makini ametumia maneno ya kudhalilisha wanawake wa nchi masikini kama Tanzania ambao ni mashabiki wa hip hop na Bongo flava. "Afande amerudi na katika singo yangu nimewaambia wasanii wabadilike, watu wanaimba vitu ambavyo ni aibu mbele ya jamii halafu wanaishia kujisifu kwamba wao ni mabingwa kwenye huu muziki,"anasema msanii huyo ambaye mtoto wake wa kwanza anaitwa Tunda.