UNALIJUA HILI/ DID YOU KNOW THIS?

POLENI NDUGU ZETU!!

GONGO LA MBOTO
1. Pu! pu! pu! hatukujua, tulidhani eti mwizi,
Kumbe ndiyo yanatua, yanatutoa machozi,
Kamwe mi sikujua, ilikua kama mionzi,
Poleni Gongo la mboto, si tupo pamoja nanyi.
2. Jeshini yalianzia, tatu usiku majira,
Watoto wanasinzia, joto la pwani si bara,
Vishindo tulisikia, tena vya mara kwa mara,
Poleni Gongo la mboto, si tupo pamoja nanyi.
3. Rais ahutubia, ni janga la kitaifa,
Wenzetu wameumia, wengine ndo wamekufa,
Serikali hudumia, maziko ya waliokufa,
Poleni Gongo la mboto, si tupo pamoja nanyi.
4. Watoto walipotea, wamama walisumbuka,
Wengine walikimbia, maafa kuyaepuka,
Mbali walikimbilia, mabomu yapolipuka,
Poleni Gongo la mboto, si tupo pamoja nanyi.
5. Pole zangu nawapeni, nduguzo mlopoteza,
Jeshi letu hongeleni, mabomu kuyatuliza,
Ilobaki walipeni, wote mali lopoteza,
Poleni Gongo la mboto, si tupo pamoja nanyi.
6. Mwishoni namtukuza, Muumbaji maanani,
Tanzania kuikuza, ndo kisiwa cha Amani,
Maadui kufukuza, wasiopenda Amani,
Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania.
Mtunzi ni dogojohnson wa blogspot.com