UNALIJUA HILI/ DID YOU KNOW THIS?

DIWANI YA MATEMBO

WAJU WAJI

1. Katika nchi hii, ya amani, wema na chuki,

Kifimbo ki chetu, cha busara, bila hamaki,

Utu ye kalinda, kwa furaha, si kwa mikiki,

Mbele kafikisha, kaachia, wanyonga haki,

Hapo sa ndipo, uwazimu, ukanishika.


2. Hapo sa ndipo, uwazimu, ukanishika,

Funika kikombe, si lazima, nimeshituka,

Wanatufanya si, ndo watwana, wametuteka,

Mi nikiyasema, ninabanwa, sijaridhika,

Ndipo wanadai, ni utoto, ninalopoka.

3. Kwetu masikini, kwao juu, tene vibonge,

Hoi tunalala, mafukala, mtaji genge,

Twapunga mwapita, twadanganywa, navyo vitenge,

Mkiingia tu, hamtoki, hadi vikongwe,

Sa umasikini, wao wetu, sisi wanyonge.


MBUZI (ZIVINDO)

1. Mbuzi wetu ni wanyama, kupika au banika,

Pili pili paka mama, kwako ndiyo imefika,

Akichingwawajituma,shughuri kushughurika,

Nyama choma yake tamu, uzuri inanukia


2 Kalete sa ile mbuzi, mapishi yataka anza,

Kaa chini kuna nazi, ukishindwa nakufunza,

Usifanye ka bazazi, kukimbia kule mwanza,

Raha ya nazi kukunwa, tena kukunwa kwa mbuzi.


JINA LANGU

1. Jina langu fahamika, kwa ndege na buibui,

Ukiita lasikika, nani sa alitambui?

Jina langu


  1. Asili ya jina langu, uzunguni la tokea,

Kutoka kwa babu yangu, mimi nikalipokea,

Jina langu.


  1. Hapo mwanzo sikujua, ujumi wa jina langu,

Nikaanza kupekua, kupata asili yangu,

Jina langu.


  1. Nikagundua machache, tena yaliyo mazuri,

Nina wapa kwa uchache, muone huo uzuri,

Jina langu.


  1. Wachache tunamiliki, na wote ni mashuhuri,

Mungu ndo katubariki, katupiga na mihuri,

Jina langu.


  1. Tukisema kinakua, tukipanga twatimiza,

Uongo twaukimbia, ukweli twautukuza,

Jina langu.


  1. Lilishika urais, tena huko Amerika,
Likaongoza weusi, nasi sa tumekomboka,

Jina langu.


  1. Mwenyewe ukiniona, mkono utaniunga,

Hatupendi kunong’ona, hatutukuzi ujinga,

Jina langu.


  1. Tunapenda kujituma, kuvuna tulichopanda,

Hatupo kilele mama, kibaya tunakiponda,

Jina langu.


  1. Wajanja ka mbayuwayu, wa akili za ziada,

Hatunywi kwenye kibuyu, na watu wanatupenda,

Jina langu.


  1. Hatukubali kutishwa, tukianza mapambano,

Hatuwezi kukatishwa, hatupendi malumbano,

Jina langu.


  1. Usikubali kuitwa, jina lisiloasili,

Kwani hutaja liteswa, kwa kukosa maadili,

Jina langu.


  1. Shida zitaja kutesa, jina litakuathiri,

Tunapotoa majina, tuangalie maana,

Jina langu.


  1. Wenye jina kama langu, sifazo nawamwagia,

Nitawapa na wanangu, waweze kujivunia,

Jina langu.


MAMA

1. Kina mama mpo wapi?

mmelala?

mnapika?

mnalea?

Mbona nyuma mnaachwa?

  1. Kina mama mpo wapi?

mashuleni?

mnasoma?

vijiweni?

Mbona huku siwaoni?

  1. Kina mama mpo wapi?

visimani?

mashambani?

mkutanoni?

Mbona hivyo kulikoni?

  1. Kina mama mpo wapi?

mahospitalini?

michezoni?

wizarani?

Mbona nako siwaoni?

5. Kina mama mpo wapi?

mabungeni?

migodini?

safarini?

Mbona kimya jamani?

  1. Kina mama mpo wapi?

unganeni?

jikomboeni?

tuongozeni?

Mbona nanyi mnaza.


KOTI

1. Nalibeba hili koti,

Koti lisilo manufa,

Nimechoka na magoti,

Hata chini ninakaa.


2. Koti langu mashuhuri,

Kagera limeshaenda,

Limepigana ukweli,

Kila mtu alipenda.


3. Koti hili lanilinda,

Nisinyeshewe na mvua,

Lashindwa kunikataza,

Nisivae kwenye jua.


4. Miyakae nenda rudi,

Koti hili nalivaa,

Lanuka kiudi udi,

Ni zuri ninapo amka.


5. Lenyewe linaniona,

Limekaa halisemi,

Nashindwa kujiongoza,

Lapenda laha sijui?


6. Tatizo lake moja tu,

Oga kama mbayuwayu,

Haliwezi kuthubutu,

Mateso kuyaondoa.


7. Siteseki peke yangu,

Chawa wanywa damu yangu,

Hata pia ya wenzangu,

Koti lawafumbatia.


8. Kunguni nao papasi,

Wapo chini yake Koti,

Koti halijitambui,

Mwilini ninapowashwa.


9. Najikaza kisabuni,

Na huo huo uduni,

Ntaliacha asilani,

Koti lisilo manufaa.


10. Mwananchi nalivaa,

Eti indo linanilinda,

Nikigoma laniponda,

Hali yangu bado duni.


11. Nayataka mapinduzi,

Koti linipe ujuzi,

Hili lilienda kozi,

Tena ile ya kijeshi.


KWENU NINYI

Nilimuona mshamba, huyu tena wa zamani,

Anabisha bila kamba, hajui wake undani,

Wa zamani ni ushamba, Kiswahili si thamani,

Kiswahili kinabamba, tena na cha ushindani.


Yeye anajua haki, hatuponda waswahili,

Mdomo wake haswaki, matusi yameshamili,

Kiswazi hakina haki, aongea kwa akili,

Kiswahili kinabamba, tena na cha ushindani.


Sijui umesikia, we bwege umepotoka,

Najua soma sheria, tusije tukakucheka,

Somo lako fatilia, usikae kuropoka,

Kiswahili kinabamba, tena na cha ushindani.


POLENI

Poleni huko mbagala, kilio kilitufika,

Salama pale mahala, ndo hivyo yakalipuka,

Silaha ndo yake ghala, vibaya yakalipuka,

Poleni huko mbagala, kilio kimewafika.

Kwanza nilipo sikia, mbio nilizitimua,

Nyuma sikuangalia, watoto waliumia,

Vilio navisikia, vumbi ju latimkia,

Poleni huko mbagala, kilio kimewatufika.


Watoto waliumia, wengi walikuwa shule,

Wengi wazidi mia, pamoja nawapa pole,

Vilema vyawaingia, sababu mabomu yale,

Poleni huko mbagala, kilio kimewafi


Wazazi walichanganya, acha mwana beba bata,

Usicheke nakukanya, usiombe kuipata,

Watu walikua nyanya, dhoruba waliipata,

Poleni huko mbagala, kilio kimewafika.


Nawaombea kwa Mungu, apokee marahemu,

Walokufa kwa uchungu, wapunguze kisehemu,

Nao walobaki ndugu, warudi kwenye sehemu

Poleni huko mbagala, kilio kimewafika.


KILIO

1. Kila kona tunalia,

majumbani,

michezoni,

makanisani,

Sababu ya kilio tunaifahamu?

2. Kila kona tunalia,

maofisini,

mashuleni,

masokoni,

Sababu ya kilio tunaifahamu?

3. Kila kona tunalia,

vijijini,

mijini,

majijini,

Sababu ya kilio tunaifahamu?



GWANDA LA JESHI

Afrika masikitiko, kila kona sa ni fujo,

Hakuna madikodiko, ndelemo wala vifijo,

Pande zote ni maziko, matumbo sa alijojo,

Viongozi wa maisha, watawala i Africa,

Waongoza bila kwisha, na mipini wameshika,

Makali yasiyo kwisha, wananchi ndo tumeshika,

Sudani nao wakongo, wanawake wateseka,

Vunja yao migongo, wanabakwa kadharika,

Wengine sa ni waongo, wanaume surubika,

Viongozi wa uongo, madaraka wameshika,

Tuache mbaya fikira, kutawala kwa maisha,

Tuache mbaya fikira, ya Mobutu na Bokasa,

Tuongoze siyo kula, na watoto kuwaasa,

Tuwapishe mabikira, wafurahie maisha,

Tupigiwe zetu kura, demokrasia kudumisha,

Uongozi imalika, demokrasia tukishika,

Bara litaheshimika, sa kote tutasifika,

Ulaya na Amerika, Asia tutasikika,

Gwanda la jeshi hatari, maendeleo Afrika.


KWETU NI PAZURI SANA

  1. Kwetu pazuri sana,

Wageni wanapishana,

Hakuna wa kulumbana,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Ila tunaibiana,

Wakaka kwa wasichana,

Kwa nini twaibiana?,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Sura zimekunjamana,

Kama ngiri wa savana,

Vya moyoni tunafichana,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Hakuna kuelezana,

Ukikosa wakazana,

Hata kama vya dhamana,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Ndiyo ni pazuri sana,

Tena matajiri sana,

Vivutio vingi sana,

Kwetu ni pazuri sana


  1. Leo nimeanza kwetu,

Kuwafunua wanetu,

Wawajue babu zetu,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Walofanya pindi yetu,

Ya kale na zama zetu,

Vijuzwe vilembwe vyetu,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Bwanyenye katutawala,

Kila kitu amekula,

Kabwela njaa twalala,

Kwetu ni pazuri san


  1. Kadela nyosha mkono,

Nijue ka ndani umo,

Usije vunja kiuno,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Usije vunja kiuno,

Kwani mmejaa mno,

Mmebanana kimshono,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Ndiyo mmejaa mno,

Tena kama konokono,

Kwenye shimo lenye choo,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Mmelala kama pono,

Mmekunja na mikono,

Hewa si tena mololo,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Sioni nitapopita,

Leba mmejikunyata,

Hadha hi mnaipata,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Huku kweli mnajuta,

Sakafuni kujikuta,

Matumbo mwayafumbata,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Vichanga vikizaliwa,

Wengine ndo waibiwa,

Wachache wasingiziwa,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Vibonge wananenepa,

Maovu wanayafupa,

Ukiomba hatokupa,

Kwetu ni pazuri sana.

  1. Wamama wamejilaza,

Huko leba wamejaza,

Vibonge wanawabeza,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Shidazo wanazipata,

Huwezi kuzikamata,

Wahusika wajinata,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Vifo vitazuilika,

Kina mama falijika,

Na watoto kadharika,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Jamani vibonge vipo,

Vinakula letu jasho,

Nasema kule walipo,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Nasema kule walipo,

Kwetu wanajaa kopo,

Wanakula vya makopo,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Ukiomba hato kupa,

Sababu tu ni mfupa,

Wenye nyama kama papa,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Kabwela wanaumizwa,

Kila kukicha walizwa,

Wakiiba wakimbizwa,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Kabwela hana haki,

Kwenye nyumba yenye chuki,

Akisema hasikiki,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Hana anacho miliki,

Ni hoja ya kudhihaki,

Kabwela mjenga nchi,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Uoga unatuponza,

Kuna kitu twajifunza,

Ipo siku tutafunza,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Kweli ni pazuri sana,

Amani imeshonana,

Ila ya uoga sana,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Vizuri vimejazana,

Wachache wamegeana,

Tena matajiri sana,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Muda mwingi mi nawaza,

Moshi tunaufukiza,

Ipo siku utawaka,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Siku hiyo ukiwaka,

Tutakipoteza kiza,

Tumechoka zulumika,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Ndiyo tutatokomeza,

Wanacho jificha kiza,

Tutaanza kumulika,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Tabu hizi zitakwisha,

Hari tutaiamsha,

Tutakuwa na bashasha,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Hakuna pa hauweni,

Madukani na sokoni,

Popote changanyikeni,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Unabisha si pazuri?,

Mabwana wala vizuri,

Watwana yetu sifuri,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Moja tisa sita moja,

Tuliujenga umoja,

Vitu vyote kwa umoja,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Kifimbo kilitikisa,

Kukomboa kisiasa,

Hakikupenda usasa,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Madaraka akaacha,

Kuwapisha kina chacha,

Kweli kamwaga pakacha,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Kweli pakawa chakacha,

Sa pakaanza kuchacha,

Yao fungua makucha,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Sifichi haya hakika,

Maovu yakaibuka,

Sijui ka tutafika,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Nasema kweli hakika,

Kifimbo kilichukika,

Mwishoni kikaanguka,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Ndo basi kilianguka,

Kwetu kukabadilika,

Nyumba ikaharibika,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Mambo yamebadilika,

Kuliko tulikotoka,

Kwa kweli nasikitika,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Wanangu nimechukika,

Uchu uliongezaka,

Chuki haikuzeeka,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Undugu uliibuka,

Ukabila ulizuka,

Pakawa ni patashika,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Umoja ulitoweka,

Uroho ulituteka,

Mizizi ilisimika,

Kwetu ni pazuri sana.

  1. Bado mngali vijana,

Nawafunza sa kuona,

Nyumbani pagumu sana,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Nawafunza sa kuona,

Ya ndani tena kwa kina,

Msije mkakosana,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Wanangu mwalithi nini?,

Nikienda kaburini,

Nawaacha masikini,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Sisi wakuwa si hivi,

Ubinafusi na wivi,

Vyatufanya kuwa hivi,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Siri moja sikieni,

Wanangu sa amkeni,

Nanyi sa chekelehani,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Ndiyo sa nanyi chekeleheni,

Mlivyo jivunieni,

Ushindi aminieni,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Ushindi aminieni,

Ipo siku sindaneni,

Mabwana wabishieni,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Mabwana wabishieni,

Kwa hoja wakataeni,

Zilizo kuntu semeni,

Kwet ni pazuri sana.


  1. Shida hizi zitapita,

Uoga mtaufuta,

Mtakuja kwa utata,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Wao tu wafaidike,

Na sisi tuhangaike,

Mwishowe ndo watucheke,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Mwishowe ndo watucheke,

Mjinga yake mateke,

Punda mizigo atwike,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Kumbuka mbuzi wachunga,

Ng’ombe pia wazichunga,

Kondoo umezifunga,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Zote tabu umepata,

Malishoni kutafuta,

Wakati sa umefika,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Vitamu nasi tuvinywe,

Kwani si vyao wenyewe,

Wanywe wao si tulewe,

Kwetu ni pazuri sana.

  1. Mlimani mkapanda,

Kwa tabu ndo mkashinda,

Makungwi wakawafunda,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Uzuri mkaukuta,

Uozo mkaupata,

Uvundo ukawatupa,

Kwetu ni pazuri sana.

  1. Miezi hamkumaliza,

Pipa sa mkalipanda,

Mkaruka kama kinda,

Kwetu ni pazuri sana.

  1. Mwastaabisha wanangu,

Mwayakimbia machungu,

Njoo mtoe ukungu,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Kazi bila manufaa,

Nani atakutendea,

Kungwi hakunihusia,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Kwetu mapesa ndo mbele,

Kukata kihelehele,

Ukanunue mchele,

Kwetu ni pazuri sana.

  1. Huna mbele wala nyuma,

Hapa kwetu huta chuma,

Hutabaki guma guma,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Hutabaki guma guma,

Wenzako wanasukuma,

Maisha si lele mama,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Maisha si lele mama,

Upepo unapovuma,

Elekea utachuma,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Lala lala na uzikwe,

Ukiamka uchekwe,

Tembea mwana kwerekwe,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Mapapai ndo mabivu,

Hatuyapaki majivu,

Usiweke na uvivu,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Utayala na uchoke,

Nako kwenu usifike,

Ukalala cheke cheke,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Huku mshike mshike,

Wanaume kwa wakike,

Mambo yote yeke yeke,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Sokoni yajazwa tele,

Na mengine kwa kelele,

Yatoka vipele pele,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Uroho utakuponza,

Uharo utakufunza,

Mara moja utaanza,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Mengi yao yameoza,

Njiani yamejilaza,

Kwe shepu yana kimbiza,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Bei yake si ya ghari,

Yapo uwanja wa fisi,

Mtaji yanafilisi,

Kwetu pazuri sana.


  1. Ukiyala huto acha,

Utapenda kupikicha,

Tena usiku wa kucha,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Yatafanyaje yameshindwa,

Majumbani yamedundwa,

Yamekimbia kufundwa,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Buguruni kwa malapa,

Mapapai utapata,

Ohio ukija pita,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Mengi yao ni jioni,

Ofisi barabarani,

Mtaji wa masikini,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Bei yake mapatano,

Mengine ya mia tano,

Ukiyacheki manono,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Mengine madogo mno,

Yamekimbia masomo,

Kama si hicho kilimo,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Mengi yao yameoza,

Mithiri ya yai viza,

Muzaji hato kujuza,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Muzaji hato kujuza,

Kama yake yameoza,

Madawa ayapuliza,

Kwetu ni pazuri sana.

  1. Mabinti twawapoteza,

Taifalo lateleza,

Shimoni twaliingiza,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Shimoni twaliingiza,

Nguvuzo twazioteza,

Ujinga kuendeleza,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Ujinga kuendeleza

Wana kuwaangamiza,

Kisacho tuliteleza,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Sa nani atawajuza,

Hao waliopoteza,

Huko walikoteleza,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Vibopa wautazama,

Udharimu kutokoma,

Mbeleni kuusukuma,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Ni lini tutaja koma,

Kila mtu kujituma,

Biashara ije koma,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Hii yategemeana,

Wavulana wasichana,

Kwa pamoja kupambana,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Ukishangaa ya Musa,

Nduguyo watakukosa,

Ninyi wanagu wa sasa,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Nyumbani moshi wafuka,

Babu tulisha mzika,

Nani sa atasikika,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Nani sa atasikika,

Kuongea eleweka,

Hakubali kuyumbika,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Mambo ni ya mgongano,

Hakuna maelewano,

Kukicha maandamano,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Kweli ni maandamano,

Ya kupinga mapunjano,

Wenye kisu kama meno,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Si kitu kipya chazuka,

Ni ulembo wa Tambuka,

Mwana asiye pulika,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Vaa mdala wa vandu,

Hata mgosi wa ndugu,

Bila kujali madudu,

Kwetu ni pazuri sana.


  1. Msichana apendeza,

Mvulana achukiza,

Vipini kujitoleza,

Kwetu ni pazuri sana.


100. Tumeiga Amerika,

Kumbe ndo tunapotoka,

Bila maana kujulika,

Kwetu ni pazuri sana.


101. Kila kitu na maana,

Wavulana wasichana,

Pambo mjue si lana,

Kwetu ni pazuri sana.


102. Dada kavaa kikuku,

Mguuni kama kasuku,

Kupita huku na huku,

Kwetu ni pazuri sana.

103. Ndiyo! kaiga masai,

Kumbuka havai cheni,

Shanga zao mguuni,

Kwetu ni pazuri sana.


104. Kumbuka kwetu vibopa,

Tena mafisadi papa,

Kamwe siwezi ongopa,

Kwetu ni pazuri sana.

105. Hakuna cha kuogopa,

Ukweli huu nawapa,

Wezi ndiyo tunawapa,

Kwetu ni pazuri sana.

106. Tunawapa kuongoza,

Ndo mana watubuluza,

Mali zetu wanauza,

Kwetu ni pazuri sana.

107. Kwenye kura anatupa,

Mlungula anawapa,

Uongozi mnampa,

Kwetu ni pazuri sana.


108. Uongozi mnampa,

Huyu nyangumi si papa,

Kwenye kura anapepa,

Kwetu ni pazuri sana.


109. Kumbukeni kule EPA,

Yalipofika mapapa,

Pamoja mliwakwepa,

Kwetu ni pazuri sana.


110. Wanangu mlishafika,

Kwenye FEDHA tunaweka,

Ukabila wajitweka,

Kwetu ni pazuri sana.


111. Kwa ulinzi imalika,

Na tena kunasifika,

Kule ndo kuliibika,

Kwetu ni pazuri sana.


112. Yule nyangumi wa EPA,

Hadi leo anapeta,

Nani atamkamata,

Kwetu ni pazuri sana.


113. Iba wewe usikike,

Uzione yekeyeke,

Na moto ukulipuke,

Kwetu ni pazuri sana.


114. Mwenye FEDHA hana HAKI,

Masikini yake chuki,

Mwalimu anahamaki,

Kwetu ni pazuri sana.


115. Mwalimu ana hamaki,

Haipati yake haki,

Kutwa yupo kwenye chaki,

Kwetu ni pazuri sana.