Siku za hivi karibuni hapa chuoni Makumira University kuna bonge la mchezo wa hatari unaoendeshwa na wajinga wachache ambao kwa ajili ya usalama wao majina yao nayawaweka kapuni wameanzisha mtindo wao ambao "wanakufuata kama mshikaji wao na kisha wanakuita pembeni hata kama ulikua na michingo ya ukweli so unaamua kuwafuata kisha wanakuambia mambo ya ajabu ajabu kuwa...nanukuu eti mwana una virusi vya ukimwi (NGOMA) na wanakuthibitishia kuwa wameambiwa na mshikaji wao wa karibu ambaye anatoka karibu na home kwenu then kwa huakika zaidi wanafanya kama wanampigia simu na kuweka loud speaker ili na wewe usikie na kweli unasikia sauti ya msela kama wewe ni mvulana na sauti ya demu kama wewe ni msichana kumbe sauti hiyo wanakua wameirekodi kwenye simu zao kisha wanaanza kukubeza kuwa unga miwaya na umekuja huku kuisambaza........" wadau msipime kama una roho ndogo unaweza kumpeleka mtu polisi so kaeni makini na mchezo huo ambao kwa hapa chuoni umeenea kwa sana.
KAENI NAO CHONJO JAMAA HAO!!